Hatimae uongozi wa klabu ya Real Madrid umekubali kumuuza mlinda mlango Iker Casillas kwenye klabu ya FC Porto na wakati wowote kuanzia leo unatarajia kuthibitisha kukamilika kwa dili hilo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa kwenye gazeti la Marca la nchini Hispania, zinaeleza kwamba tayari viongozi wa klabu hizo mbili wameshafikia makubaliano na kilichosalia ni kuweka mambo hadharani.

Casillas, ameingia katika mchakato wa kuuondoka Stantiago Bernabeu baada ya kuonekana huduma yake haihitajiki kwa sana kama ilivyokua miaka ya nyuma, kwa madai kiwango chake kimeporomoka.

Meneja Jose Mourinho, anatajwa kuwa chanzo cha kubaini mapungufu ya mlinda mlango huyo aliyedumu klabuni hapo kwa zaidi ya miaka 20, kwa kumnyima nafasi ya kukaa langoni na nafasi yake kuchukuliwa na Diego López Rodríguez miaka mitatu iliyopita.

Diego López Rodríguez alisajiliwa na Jose mourinho akitokea Sevilla CF na alionyesha kuitumikia ipasavyo nafasi ya kuaminiwa kukaa langoni mwa klabu hiyo na kufanikisha azma ya kutwaa ubingwa wa nchini Hispania.

Mipango ya kuondoka kwa Casillas, inaibua upya mikakati ya kusajiliwa kwa mlinda mlango wa klabu ya Man Utd, David de Gea ambaye kwa sasa ameshajumuika na wachezaji wenzake wa mashteni wekundu kwa maandalizi ya msimu mpya wa ligi.

Casillas, alikuzwa na kituo cha kulea vipaji cha Real Madrid kuanzia mwaka 1990–1998 na baada ya hapo alipandishwa kwenye kikosi cha Real Madrid C kuanzia mwaka 1998–1999, ambapo alicheza michezo 26 kabla ya kujiunga na kikosi cha Real Madrid B mwaka 1999 na kisha alipelekwa kwenye kikosi cha wakubwa cha klabu hiyo, na mpaka sasa ameshakitumikia katika michezo 510.

Majina Matano Mbele Ya NEC Leo
Tailor Swift Asaidia Kuokoa Maisha Ya Mtoto Anaeteswa Na Leukemia