Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF), Shirika la Biashara Duniani -WTO yameonya kuwa sera za Marekani za kujilinda kibiashara zinaweza kuwa na athari kwa uchumi wa dunia,
Onyo hilo limetolewa katika mkutano ulioItishwa na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel na viongozi wa mashirika ya kimataifa jijini Berlin.
Merkel ambaye alikuwa miongoni mwa viongozi wa nchi waliohudhuria mkutano wa nchi saba zenye nguvu kiuchumi na biashara duniani G-7 nchini Canada wiki iliyopita, ambapo amesema kuwa wale waliokuwa kwenye mkutano huo, walikuwa na shauku ya maendeleo endelevu ya uchumi ulimwenguni kupitia ushirikiano.
Aidha, amesema kuwa uamuzi wa utawala wa Trump wa kutoza ushuru mpya wa bidhaa za chuma cha pua na bati uko kwenye hatua ngumu na yenye utata.
Hata hivyo, mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wa Shirika la Fedha Ulimwenguni IMF, Shirika la Bishara dunia WTO, Shirika la Ustawi wa Kiuchumi na Maendeleo, Benki ya Maendeleo ya Afrika pamoja na Shirika la Kazi Duniani ILO.