Wananchi nchini Italia wameanza mchakato wa kumbaini na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria mtu au taasisi ambayo wanaamini ni sababu ya mlipuko wa virusi vipya vya corona (covid-19) nchini humo.

Aidha waendesha mashtaka nchini humo wanaendelea kufanya uchunguzi kubaini makosa yaliyofanywa na wenye Mamlaka ambayo wanaamini yalichangia ongezeko la mlipuko wa virusi hivyo.

Wakurugenzi wa kituo kimoja cha afya ambapo wagonjwa wa corona walifariki dunia, wako hatarini kufunguliwa mashtaka ya kuua bila kukusudia.
Italia ndiyo nchi ya pili kwa idadi kubwa ya visa vya corona barani Ulaya ikiwa na visa takriani 190,000 nyuma ya Hispania yenye visa 213,024. Marekani ndiyo inayoongoza duniani ikiwa na visa vilivyothibitishwa zaidi ya 886,709.
Kwa mujibu wa CNN, zaidi ya watu 45,000 ambao ni ndugu wa waathirika wa virusi vya corona wameanzisha kampeni kwenye mtandao wa Facebook yenye jina ‘NOI denunceremo’, ikimaanisha ‘tutaanika maovu yako’.
Katika hatua nyingine, jana, Aprili 23, 2020, Chancellor Angela Markel wa Ujerumani aliwaonya Magavana wa majimbo ya nchi hiyo kuwa kulegeza masharti kunaweza kuvuruga hatua iliyopigwa katika kupambana na kusambaa kwa virusi vya corona.

Hadi sasa kuna jumla ya visa Milioni 2.71 vilivyothibitishwa duniani kote, wagonjwa 743,000 wamepona na 191,000 wamepoteza maisha, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani.

Jela maisha kwa kumbaka mtoto wa miaka 8

RC akemea taasisi za mikopo kutapeli wastaafu Rukwa

Serikali yakemea Trafiki kujificha vichakani na kupiga picha za magari kwa simu
Dar kinara ukusanyaji wa mapato nchini