Mkuu wa mkoa wa Katavi, Juma Zuberi Homera amezitangazia Vita taasisi zinazotoa mikopo katika mkoa huo na kuwatapeli walimu mafao yao baada ya kustaafu.

Homera ametoa kauli hiyo Mara baada ya kumkabidhi mwalimu Renatus Ngailo nyumba aliyoipata kutokana na kurudishiwa pesa aliyotapeliwa na taasisi moja ya mikopo iliyopo mkoani humo baada ya kupokea mafao.

Mkuu wa Takukuru mkoa wa Katavi Christopher Nakua amesema, mnamo march 18 mwaka huu walipokea malalamiko kuwa mwalimu Charles Nyansio na mwenzake Renatus Ngailo wamedhulumiwa fedha za mafao yao ya kustaafu.

Amesema Nyansio alikopa kiasi cha sh 12,000,000 kwa nyakati tofauti kutoka kwa mkopeshaji na baada ya mafao yake kutoka walichuku kiasi cha sh 50,000,000 kutoka kwa Mwalimu huyo.

Amesema mkopeshaji huyo alichukuwa kadi yake ya benki na namba yake ya siri hivyo aliendelea kuchukuwa mafao ya kila mwezi kwa muda wa miezi 3 na kufanikiwa kuchukuwa kiasi cha sh 300,000 kwa kila mwezi hadi pale mwalimu huyo alipobadili akaunti ya kupitishia mafao yake.

Uchunguzi ulipofanyika mtuhumiwa alikiri makosa na kumrejeshea mlalamikaji kiasi cha sh 20,000,000 ambapo fedha hiyo ilikuwa kama dhuluma kwa mlalamikaji kwa kutokuwa na maelezo ya kutosha.

Mstaafu huyo alikabidhiwa pesa taslimu sh 5,000,000 na kiasi cha sh 15,000,000 alipewa nyumba na mtuhumiwa huyo iliyopo maeneo ya Kawajense ambayo amekabidhiwa Jana na mkuu wa mkoa.

Kwa upande wake Renatus Ngailo na mwl Charles Nyansio ambao ni wastaafu kwa pamoja wameishukuru taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) na serikali ya mkoa wa Katavi kuhakikisha haki za wanyonge zinapatikana.

Jela maisha kwa kumbaka mtoto wa miaka 8
EU yaonya matumizi ya dawa za Malaria kutibu Corona