Mamlaka ya dawa ya Umoja wa Ulaya imeonya kuwa dawa za malaria zinazotumiwa kwa majaribio kutibu ugonjwa wa covid-19, zinaweza kusababisha madhara makubwa, ikiwemo kifafa na matatizo ya moyo.

Mamlaka hiyo imesema katika taarifa yake kuwa dawa za Chloroquine na hydrxychloroquine, zinazopigiwa upatu na watu wengi kama zinazoweza kuwa tiba ya covid-19 , zinajulikanakwa kusababisha matatizo ya mapigo ya moyo, hasa inapochanganywa na dawa nyingine.

Dawa za chloroquine na hydroxychloroquine zimetumiwa kwa muda mrefu kutibu malaria, na magonjwa ya maumivu. Mbali na uwezekano wa kusababisha matatizo ya moyo, dawa hizo mbili zinaweza pia kuwa na madhara mengine yakiwemo kuharibu ini na figo, na pia kusababisha kushuka kwa sukari mwilini.

Mpaka sasa hakuna tiba iliyoidhinishwa kwa ajili ya covid-19 na majaribio kadhaa yanaendelea kote duniani…bofya hapa kujua matokeo ya jaribio la dawa ya kwanza Jaribio la kwanza dawa ya Corona limefeli

RC akemea taasisi za mikopo kutapeli wastaafu Rukwa
Jaribio la kwanza dawa ya Corona limefeli