Marehemu Kanumba katika moja ya filamu zake amewahi kutumia msemo unaosema mwanzo wa mapenzi huwa mtamu kama asali ila mwisho wa mapenzi huwa mchungu kama shubiri.

Baada ya penzi la Wolper na Harmonize kuvunjika, kupitia mitandao yao ya kijamii wamerushiana vijembe vikionesha kila mmoja alikuwa anamvumilia mwenzake pindi walipokuwa katika penzi zito, ambapo Rajab Abdul maarufu kama Harmonize ametumia sanaa yake ya muziki kumfikishia ujumbe Jackline Wolper kwa kutumia wimbo unaenda kwa jina ‘Nimechoka’.

Timbwili hilo limeanza jana ambapo Harmonize alitupia baadhi ya mistari katika wimbo wake Nimechoka vilivyogusa maisha yake na Wolper ambapo kwenye Instagram aliandika hivi jana.

‘’Naomba nikupe jukumu la kumtumia Ex wako ambaye kila kukicha anakuzungumzia tena kwa ubaya na kutengeneza mazingira ya kukujengea chuki katika jamii…..na umwambie Nimechoka …Ukiweza mtag…Zawadi’’.

Wolper hakuweza kuvumilia shambulio hilo naye aliandika waraka mrefu kwa Harmonize, na kuijibu  baadhi ya mistari katika wimbo huo.

”Tusilazimishane kuongea nimeshaachana na wewe kiusalama ongelea vilivyopo kwako saivi sio mimi, Nilishatokaga huko kirahisi unaweza ukadeal na style yako ya mziki bila kunihusisha maana unampa hofu pia BFF anahisi labda kuna kitu kumbe hakuna, usiniharibie mahusiano yangu mapya , BFF wangu ni bora kuliko wewe ni adimu na sitaki kumpoteza kwa ajili ya watu kama wewe…Mimi ni Jackie Wolper ambae siwezi kuacha kuongea ukinianza namaliza kwa wale wanaosema bora kunyamaza subirini yawakute alafu mjipe huo ushauri”. Ameandika Wolper kupitia mtandao wake wa instagram.

Baada ya povu la Wolper, Harmonize ametupia video instagram akiwa anampikia mpenzi wake mpya, Sarah video hiyoo imesindikizwa na maneno haya.

Vipi kwani??? mbona nasikia mtaa wa 3 povu kwani katajwa mtu?? ukweli unaumaga ..Nimechoka.. mwambie tena anajifanya anakujua sana !! pambana na hubalako”.

Toa maoni yako nani yupo sahihi, je nani yuko Sawa kati ya Jackline Wolper na Harmonize.

 

 

 

WCB waja na hizi mbili ''Nishachoka na Unaibiwa''
Paul Pogba kuikosa Everton jumapili