Jamhuri ya Demokrasia ya Congo bado inakabiliwa na janga la ugonjwa wa mlipuko wa Ebola na hii imethibitishwa baada ya kutokea kwa kesi mpya ya mtu mmoja kufariki dunia kwa ugonjwa huo siku ya Alhamisi baada ya kipindi cha siku 52 zilizopita kuwa hakuna kesi ya ebola iliyoripotiwa nchini humo.

Taarifa hiyo imetolewa siku ya Ijumaa na Shirika la Afya Duniani (WHO) baada ya kuthibitisha kutokea kwa kisa hiko cha Ebola huko Jamhhuri ya Kidemokrasia ya Congo zikiwa zimesalia siku chache tu kabla ya kutangazwa rasmi kumalizika kabisa ugonjwa huo nchini humo.

”Ni bahati mbaya kwamba Serikari ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo haiwezi kutangaza rasmi kuwa janga hilo la Ebola limekwisha nchini, kama ilivyopangwa kutangazwa siku ya jumatatu” Amesema Dk Tedros Adhanom, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Waziri wa Afya amesema kuwa ripoti hiyo inaonyesha aliyefariki ni kijana mwenye umri wa miaka 26 na tayari wanashirikiana na WHO kufanya uchunguzi wa kina ili kufahamu kama kuna wagonjwa wengine.

Kwa mujibu wa takwimu za WHO katika ukurasa wa Twitter limechapisha kuwa zaidi ya watu 2,273 wamefariki dunia na kufanya ugonjwa huo kushika nafasi ya pili katika magonjwa ya mlipuo yaliyoua zaidi watu duniani.

Aidha, tangazo la kugunduliwa kesi hiyo mpya limekuja zikiwa zimebakia siku chache tu kabla ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutangaza kumalizika kabisa ugonjwa huo nchini humo.

Mbali na ugonjwa wa Ebola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekumbwa pia na maambukizi ya corona na hadi hivi sasa watu 215 wamethibitishwa kukumbwa na ugonjwa huo nchini humo huku 20 kati yao wakiwa wameshafariki dunia.

Corona Kenya: Wawili wafariki msongamano wa kupokea chakula cha msaada
Wavutaji wa sigara hatarini zaidi kupata Corona