Imeelezwa kuwa Wanawake wawili wamefariki dunia kwa kushindwa kupumua wakati mamia ya wakazi walipojitokeza kupokea chakula cha msaada kilichotolewa na Raila Odinga.

Mkuu wa Polisi eneo la Kibra, Andrew Musaisi amesema wanawake hao waliaga dunia saa chache baada ya kuchukuliwa katika kituo hicho na kupelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

Watu wengine ambao idadi yao bado haijafahamika walipatwa na majeraha madogo madogo katika tukio hilo ambapo inaelezwa pia palitokea vurugu wakati wa ugawaji na kusababisha mkanyagano.

Wavutaji wa sigara hatarini zaidi kupata Corona

Hatua hiyo ilikuwa ni kama njia mojawapo ya kuziepushia na njaa familia zisizojiweza baada ya Serikali kutangaza marufuku ya kutoka nje ili kuzuia maambukizi ya virusi vya covid 19.

Mwanasiasa Laila Odinga pamoja na mke wake Ida Odinga wamekuwa ni miongoni mwa wadhamini wengine waliosaidia kaya masikini kwa kuwagawia chakula, sabuni, vitakasa mikono pamoja na maji ili kuunga mkono juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya corona nchini humo.

Jinsi mgonjwa wa pumu anavyoweza kukabili Corona
Janga la Ebola bado laitafuna Congo, mmoja afariki dunia