Mahakama ya Milimani, iliyopo jijini Nairobi, imetupa ombi la lililowasilishwa na Mkenya Ojijo Mark kwa niaba ya watu 10,000 wakitaka Wajaluo wote waruhusiwe kujitenga na Kenya na kisha waasisi taifa lao na kujitawala wenyewe.

Ombi hilo, lilitupiliwa mbali na Jaji Lawrence Mugambi wa Mahakama ya Milimani, akisema halikuwasilishwa kwa njia inayofaa, kitendo ambacho huenda kimetoa mwanya kwa wahusika hao kurudi nyuma ili kujipanga upya.

Watu hao, waliiomba Mahakama iruhusu kura ya maamuzi kuandaliwa ili Wajaluo waamue mustakabali wao ikiwemo kujiondoa kuwa sehemu ya Kenya na badala yake waasisi taifa lao kwani wamekuwa wakibaguliwa na Serikali ya Kenya huku Jaji Mugambi akisema hawakufuata utaratibu unaohitajika wa kuwasilisha malalamiko yanayohusu masuala ya kikatiba.

“Nimeisoma notisi ya kesi pamoja na ombi la kutaka iwe kesi ya dharura lakini ameiwasilisha chini ya kifungu kisichofaa. Badala ya malalamiko ya kawaida, alifaa kuiwasilisha kesi chini ya kifungu cha masuala ya Kikatiba yanayohusu haki za kijamii. Kwa hivyo, ninaitupilia mbali mara moja,” Mugambi alimaliza.

Inonga kuikabili Young Africans
Wan-Bissaka afunguka mazito Man Utd