Mwanazuoni Mkongwe na Mwandishi wa habari nguli, Jenerali Ulimwengu ametoa ushauri wake kwa rais John Magufuli ambaye kasi yake inasifiwa kila kona.

Ulimwengu ambaye ameonesha kuridhishwa na kasi aliyoanza nayo Rais Magufuli, amemshauri kujikita katika kuunda mfumo thabiti utakaomsaidia kufanya kazi kuanzia ngazi ya juu hadi ngazi ya mtaa ili kasi yake idumu kwa kipindi chote.

Alisema mfumo huo utamsaidia kuhakikisha maagizo yanatelekezwa kwa ukamilifu kwa ngazi zote kwa nguvu ileile hadi katika serikali za mitaa kwa kuwa hataweza kutembelea kila ofisi.

“Rais hawezi kushtukiza kila ofisi nchini, kwahiyo mfumo mzuri ndio utakaosaidia kutekeleza vizuri ahadi zake kwa ukamilifu. Akitoa maagizo sasa yanashuka kutoka juu hadi chini katika mfumo huo,” Jenerali Ulimwengu aliiambia Azam TV.

Picha: Hii Ndio Zawadi Ya Uhuru Kenyatta Kwa Papa Francis Alipoingia Kenya
Nyundo Ya Hapa Kazi Tu Yawaangukiwa Wengine Watatu TRA