Kasi ya hapa kazi tu imeendelea kuwazoa baadhi ya watendaji wa serikali ambapo leo watumishi wengine watatu wa TRA wamesimamishwa kazi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametangaza kuwasimamisha kazi Anangiswe Mtafya, Nsajigwa Mwandengele na Robert Nyoni kufuatia upotevu wa makontena 349 yenye thamani ya shilingi bilioni 80 katika Bandari ya Dar es Salaam. Awali, Wazir Mkuu alielekeza watumishi hao kuhamishiwa mikoani.

Kama ilivyokuwa kwa watumishi wengine watano wa TRA waliosimamishwa jana, watumishi hao watatu hawaruhusiwi kusafiri nje ya nchi hadi uchunguzi juu ya sakata hilo utakapokamilika.

Waziri Mkuu pia alimuagiza Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Dk Philip Mpango kuwaandikia barua wote waliosimamishwa kazi ikiwa ni pamoja na aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo.

Jenerali Ulimwengu Amshauri Rais Magufuli ili Afanikiwe Kipindi Chote
Hapa Kazi Tu: Bandarini Hapapenyeki, Mengine Yanaswa