Kamanda wa Polisi wa kanda Maalumu ya Dar es salaam Kamishna Simon Sirro, amesema Jeshi la polisi limeanza rasmi oparesheni hiyo usiku wa kuamkia jana, ikiwa na lengo kusaka watu wanaoshukiwa kuwa ni majambazi wanaodaiwa kufanya matukio kadhaa ya ujambazi likiwemo lile la kuuawa kwa askari wanne waliokuwa wakienda lindoni, katika benk ya CRDB, Mbande jijini Dar es Salaam.

Aidha kamanda Sirro amesema kuwa katika oparesheni hiyo kuna watu waliouawa na wengine wanashikiliwa na jeshi hilo, lakini  hakutaja idadi yoyote ile ya waliouawa au waliokamatwa kwa sababu za kiusalama kwa kuwa oparesheni hiyo bado inaendelea.

Kuhusu taarifa za uwepo wa askari aliyeuawa, Kamishna Sirro hakuweza kuthibitisha au kukanusha na kusema kuwa taarifa kamili kuhusu oparesheni hiyo itatolewa siku ya Jumanne ya wiki ijayo.

Amewataka wananchi kuendelea kuwa watulivu, na kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kwa kutoa taarifa zitakazoweza kufichua wahalifu hao na kusisitiza kuwa jeshi hilo litawabaini na kuwatia nguvuni wote waliohusika.

Katika hatua nyingine, Sirro ameendelea kupiga marufuku maandamano ya aina yoyote yale katika mkoa wa Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya zuio la jeshi la polisi la kupiga marufuku mikutano ya kisiasa na maandamano nchi nzima.

Usiku wa kuamkia jana, hali ya taharuki iliwakumba wakazi wa Vikindu baada ya kikosi maalum cha askari kuvamia nyumba moja iliyoko eneo hilo, na kisha kuzuka kwa majibizano ya risasi kati ya polisi na wanaodaiwa kuwa ni majambazi waliokuwa katika nyumba hiyo

Mkapa;Kila Mmoja Ni Zawadi Kwa Mwenzie,Awakutanisha Lowassa Na Rais Magufuli Katika Jubilei Ya Miaka 50 Ya Ndoa Yake
Australia: Kijana Mwenye Miaka 18 Amudu Kuendesha Ndege Yenye Injini Moja