Katika jitihada za kulinda sura ya Magereza nchini Namibia, Jeshi hilo limepiga marufuku kuajiri watu wenye michoro ya tattoo mwilini mwao.
Hatua hiyo, inatokana na wasiwasi kwamba baadhi ya tattoo zilizochorwa na askari Magereza zinahusishwa na magenge ya wahalifu hivyo kuendelea kutoa ishara.
Kamishna Mkuu wa Huduma za Marekebisho ya Namibia – NCS, Raphael Hamunyela amesema tatoo zinazoonekana kwenye miili ya askari pia si taswira nzuri ya Jeshi hilo.
Amesema, sera ya uajiri nchini na kanuni za maadili zitarekebishwa ili kuhakikisha kuwa siku za usoni hakuna mtu mwenye tattoo zinazoonekana atasajiliwa katika NCS.