Beki wa Kati kutoka nchini Kenya Joash Onyango Achieng huenda akavunja Mkataba wake Simba SC, kufuatia kuwa na wakati mgumu wa kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha klabu hiyo, chini ya Kocha Zoran Maki.

Usajili wa Mohamed Ouattara umekua changamoto kwa Beki huyo aliyesajiliwa Simba SC msimu wa 2019/20 akitokea Gor Mahia ya nchini kwao Kenya.

Habari kutoka kwa mtu wa karibu na Beki huyo zinaeleza kuwa, Onyango anajipanga kuwasilisha ombi la kuutaka Uongozi wa Simba SC kuvunja mkataba wake, kutokana na kukosa furaha klabuni hapo.

Hata hivyo alipotafutwa Onyango ili kuthibitisha taarifa hizo alisema: “Kazi yangu ni kucheza soka, masuala mengine ya kimkataba ni siri yangu na uongozi, ila kama kuna lolote tusubiri tuone kama itakua hivyo.”

Onyango alikua Beki tegemeo katika Kikosi cha Kwanza cha Simba SC tangu aliposajiliwa klabuni hapo msimu wa 2019/20, akifanya kazi kwa ukatribu na Pascal Wawa aliyeondoka mwishoni mwa msimu uliopita, na baadae alifanya kazi na Beki kutoka DR Congo Henock Inonga.

Kocha Zoran Maki amekua akiwatumia Inonga na Ouattara tangu kuanza kwa msimu huu wa 2022/23, akiwachezesha katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Young Africans, Michezo ya Ligi Kuu dhidi ya Geita Gold FC na Kagera Sugar.

Kasi idadi ya waathirika VVU yashtua wengi
Hassan Mwakinyo auota mkanda wa WBO