Siku moja baada ya kutakiwa na jopo la Congress kuwasilisha kanda alizodai amemrekodi Mkurugenzi Mkuu wa FBI, Rais wa Marekani, Donald Trump amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa hajawahi kumrekodi na wala hana kanda hizo.

Aidha, hatua hiyo imefikiwa mara baada ya rais Trump kuandika kwenye ukurasa wake ‘Twitter’ kuwa siku chache baada ya kumfukuza kazi mkurugenzi huyo, ambapo ujumbe wake ulisomeka, “James Comey uwe na amani kuwa sina rekodi zozote za sauti yako kuhusu mazungumzo yetu tuliyoyafanya”

Ujumbe huo ulizua madai kuwa, Trump alimfukuza kazi Comey ili kuzuia uchunguzi kuhusu Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani mwaka jana ambao alionyesha ushirikiano wa karibu na nchi hiyo.

Hata hivyo, sakata hilo linaendelea kuchukua sura mpya kufuatia tuhuma zinazomkabili rais Trump kuwa alishirikiana na Urusi katika kampeni za uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika mwaka jana na kupelekea kupata ushindi

Jokate : Sipo tayari kuzungumzia maisha yangu ya kimapenzi, labda awe mume wangu
Magazeti ya Tanzania leo Juni 23, 2017