Klabu ya Arsenal ipo tayari kusikiliza ofa kwa kiungo Jorginho msimu huu wa joto, kwa mujibu wa Mtandao wa 90min.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alihamia Uwanja wa Emirates Januari huku Mikel Arteta akitafuta kukichangamsha kikosi chake kuelekea ubingwa wa Ligi Kuu.

Kikosi cha Arsenal kimekuwa tatizo kwa Mhispania huyo, ambaye alitegemea sana mastaa kama Thomas Partey, Granit Xhaka na Martin Odegaard katika miezi mitano ya kwanza ya msimu, na uzoefu wa Jorginho wa kushindana katika kiwango cha juu ulionekana kama nyongeza ya kukaribishwa.

Hata hivyo, usajili wa Jorginho ulionekana kama hatua ya muda mfupi tu na inaelewa kwamba Arsenal haitamzuia msimu huu wa joto ikiwa atapata nafasi ya kurejea Italia.

Kocha wa zamani wa Chelsea, Maurizio Sarri, ambaye sasa anainoa Lazio, ana nia ya kuungana tena na Jorginho kwenye Uwanja wa Olimpico, huku pia Napoli na AC Milan zimeonesha nia ya kumtaka.

Arsenal hawataki kumlazimisha Jorginho kuondoka katika klabu hiyo lakini wanafahamu kabisa kwamba wanahitaji kutengeneza nafasi kwenye kikosi chao kwa ajili ya wachezaji wanaoingia, Granit Xhaka anaondoka katika klabu hiyo na kujiunga na Bayer Leverkusen na Albert Sambi Lokonga, ambaye muda wake wa mkopo katika klabu ya Crystal Palace haukufaulu, pia huenda akatolewa.

Kuondoka kwao kunaweza kurahisisha kuwasili kwa Declan Rice na Moises Caicedo, huku Arsenal wakiwa na nia ya kusajili wachezaji wote wawili licha ya bei zao za juu.

Nahodha wa West Ham, Rice, ambaye alinyanyua taji la Europa Conference Jumatano usiku, anataka kusonga mbele ili kutimiza malengo yake lakini klabu hiyo itashikilia msimamo wao wa dau la pauni milioni 100.

Kwa upande wa Brighton, wanaweza kuwa tayari kukubali takriban pauni milioni 80 kwa Caicedo fedha ambayo Arsenal hawakuwa tayari kuitoa Januari.

Mac Allister: Ndoto iliyotimia siwezi kusubiri
Uvumi ukodishaji wa Bandari wamuibua Musukuma