Taarifa kutoka ndani ya Manchester United, inakaribia kunasa saini ya beki anayekipiga Monaco, Axel Disasi kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi.

Man United ipo sokoni ikisaka ya beki mwingine wa kati baada kupambana kwenye ligi bila ya uwepo wa Lisandro Martinez aliyeumia mguu.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na L’Equipe, Man United ipo mbioni kuinasa saini ya beki huyo aliyehusishwa na Chelsea pia.

United na Monaco zitazungumza kukamilisha dili hilo ambalo litagharimu Pauni 34 milioni hadi kufikia Pauni 43 milioni.

Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekubali kujiunga na Man united msimu ujao, anamudu pia kucheza nafasi ya kulia, anataka kutua Man United kwa sababu Monaco imeshindwa kufuzu michuano ya Ulaya msimu ujao.

Nahodha wa Man United, Harry Maguire huenda akatemwa kutokana na kukosa namba ya kudumu kikosi cha kwanza.

Ajira: Serikali kuanzisha, kuhuisha mafunzo ya Elimu
Wanasayansi watahadharisha El-nino, ongezeko la juu joto