Mshambuliaji na Nahodha wa kikosi cha Senegal Sadio Mane yupo katika orodha ya wachezaji saba ambao hawatakiwi Bayern Munich chini ya Meneja Thomas Tuchel kwa mujibu wa ripoti.

Tuchel, ambaye aliipa Bayern ubingwa wao wa ll mfululizo katika Bundesliga majuma mawili yaliyopita, anataka kujenga kikosi chake akianza na kupangua baadhi ya wachezaji.

Winga huyo aliyejiunga katika usajili wa kiangazi uliopita, akitokea Liverpool ataungana na Leroy Sane na Serge Gnabry ambao wamefunguliwa mlango wa kutokea.

Wengine ni beki Bouna Sarr, kipa Alexander Nubel na kiungo wa kati Marcel Sabitzer aliyemaliza kukipiga kwa mkopo Manchester United.

Wakati huohuo Benjamin Pavard anakamilisha orodha ya wachezaji saba baada ya kugoma kusaini mkataba mwingine wa kundelea kukiiga Bayern.

Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa ananyemelewa na FC Barcelona na Liverpool na imeelezwa anaweza kuondoka kwa sababu maalumu ambayo haijawekwa wazi endapo Bayern itapewa ofa Pauni 25 milioni.

Licha ya kumsajili Mane kwa Pauni 31 milioni, Bayern inajiandaa kusikiliza ofa kwa timu yoyote inayomuitaji.

Ufuatiliaji miradi, shughuli za Serikali wajadiliwa
Ajira: Serikali kuanzisha, kuhuisha mafunzo ya Elimu