Imeelezwa kuwa Meneja wa Klabu ya AS Roma inayoshiriki Ligi Kuu ya Italia ‘Serie A’ Jose Mourinho ameitema Ofa ya kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya taifa lake la Ureno.
Mourinho alitajwa kuwa miongoni mwa makocha wanaofikiriwa kuchukua nafasi ya Kocha Fernando Santos aliyeondolewa kwenye timu hiyo, baada ya kushindwa kufikia malengo kwenye Fainali za Kombe la Dunia zilizomalizika hivi karibuni nchini Qatar.
Meneja huyo Raia wa Ureno amewaeleza watu wake wa karibu kuwa, hayuko tayari kuondoka AS Roma kwa sasa, kwa sababu anaami kuna kazi kubwa ya kufanya Klabuni hapo.
Amesema anatambua thamani aliyooneshwa na viongozi wa Shirikisho la soka nchini Ureno ya kufikiriwa kuwa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, lakini hana budi kujikita kwenye majukumu ya klabu yake kwa sasa.
Mourinho bado anatamani kufundisha ngazi ya vilabu kama ambavyo huwa anazungumza siku zote, kuwa hatamani kufundisha timu za taifa kwa sababu hazina usajili.
Kabal ya kufutwa kazi, Kocha Fernando Santos ambaye amekua na Kikosi cha Ureno tangu mwaka 2014, aliifikisha timu hiyo hatua ya Robo Fainali katika Michuano ya Kombe la Dunia na kutolewa na Morocco kwa kufungwa 1-0.