Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemtumia salamu za rambirambi aliyekuwa Naibu Waziri na Mbunge Mstaafu wa Mpwapwa, Gregory Teu kufuatia vifo vya watu 13 ambao ni ndugu wa familia yake waliopoteza maisha katika ajali ya gari iliyotokea nchini Uganda.
Watu hao wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka kwenye sherehe ya harusi kugongana na lori katika barabara ya Masaka Kampala nchini Uganda wakiwa njiani kurejea Tanzania.
“Nimepokea taarifa ya vifo hivi kwa mshtuko mkubwa, nimehuzunishwa na kuondokewa na idadi hii kubwa ya watu, nampa pole Ndg. Gregory Teu kwa kufikwa na msiba huu mkubwa, nawapa pole wanafamilia, ndugu na jamaa wote walioguswa na vifo hivi,”amesema Rais Dkt. Magufuli
-
Siku ya mtindio wa ubongo kuadhimishwa jijini Dar
-
Lema anena mazito kuhusu waliokamatwa na polisi
-
Ukimwi wazidi kuwa tishio nchini
Hata hivyo, Rais Magufuli amewataka wanafamilia wote kuwa na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na wapendwa wao na watu muhimu waliowategemea.