Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni wataweka jiwe la msingi mradi wa bomba la kuasafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania Agosti 5, 2017.

Taarifa hiyo imetolewa leo Julai 28, 2017 kutoka Ikulu ambapo imeeleza kuwa takribani ajira 10,000 zitazalishwa katika ujenzi wa mradi huo na watanzania watanufaika kwa kiasi kikubwa, hivyo watanzania wametakiwa kufuatilia matangazo ya moja kwa moja ambayo yataonyeshwa kupitia vyombo vya habari.

 

Magazeti ya Tanzania leo Julai 29, 2017
JPM aipa tano TCU, "nataka tuwe na nchi nzuri"