Mkataba wa kiungo wa klabu ya Manchester United, Juan Mata umebakiza miezi kumi na mbili kumalizika lakini mchezaji huyo ameonyesha nia ya kutaka kubaki Old Traffold baada ya kukataa mshahara wa pauni 375,000 kwa wiki kujiunga na ligi kuu ya China.
Pamoja na kutopewa kipaumbele na kocha Jose Mourinho katika kikosi cha kwanza Mata anaonekana kuridhika na maisha ya Mancheter na huenda akaongeza mkataba kuendelea kukipiga na kikosi cha Mourinho.
”Nina furaha hapa kuwa hapa, nimekuwa hapa kwa karibia miaka minne sasa baba yangu amefungua mgahawa wa kihispania na kwakuwa mabo ni mazuri ninafurahia kubaki hapa,” alisema Mata.
- Liverpool yaishushia Maribor kipigo cha mwizi, Spurs, Madrid hakuna mbabe
-
Majeruhi yazidi kuiandama Chelsea
-
Wachezaji watano kukiongezea nguvu kikosi cha Yanga
Kiungo huyo mshambuliaji alijiunga na Manchester United mwaka 2014 kwa kitita cha Pauni milioni 37.1 akitokea Chelsea.