Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) imetoa orodha ya kwanza ya majina ya wanafunzi 10,196 kati ya wanafunzi 30,000 wanaotarajiwa kunufaika na mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka mpya wa masomo 2017/2018.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo Abdul-Razaq Badru alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema zaidi ya shilingi bilioni 34.6 tayari zimetengwa kwa ajili ya wanafunzi hao waliopitishwa.

Amesema kuwa kwa mwaka wa masomo wa 2017/2018 Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 108.8 kwa ajili ya wanafunzi hao wapya 30,000 wanaotarajiwa kujiunga na vyuo vikuu.

“Orodha ya kwanza tayari inapatikana katika tovuti ya bodi ya mikopo www.helsb.go.tz na itatumwa kwa vyuo husika. Orodha nyingine (batches) zitafuata kadri taratibu za udahili na uchambuzi zitakavyokuwa zinaendelea kukamulika,”amesema Badru

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo wa Bodi hiyo Dkt. Veronica Nyahende amesema kuwa majina ya wanafunzi wote waliokosea majina yao yatafanyiwa uchambuzi na zoezi hilo likikamilika majina yao yatatolewa.

Hata hivyo, awamu ya kwanza ya wanafunzi hao 10,196 waliopata mkopo imepatikana baada ya bodi ya mikopo kupokea na kuchambua awamu ya kwanza ya majina ya wanafunzi 32,495 waliopata udahili katika chuo kimoja, hivyo ikumbukwe kuwa sifa kuu za kupata mkopo ni mwombaji awe amepata udahili katika taasisi ya elimu ya juu inayotambuliwa na serikali.

Benchi la ufundi Simba Sports Club lameguka
Juan Mata akataa kiasi hiki cha fedha kwenda China