Meneja wa Juventus FC, Massimiliano Allegri ameionda timu yake kwenye mbio za Ubingwa wa Ligi Kuu Italia ‘Serie A’, baada ya kupokea kichapo cha 1-0 dhidi ya Inter Milan mwishoni mwa juma lililopita.

Allegri amesema matokeo ya kupoteza mchezio dhidi ya Inter Milan yanaashiria mwisho wa matumaini ya Juventus FC kuwania taji la Ligi Kuu ya Italia ‘Scudetto’, msimu huu 2021/22.

“Kuanzia sasa tunaweza kusema kwamba Juventus wametolewa kabisa kwenye mbio za Scudetto,” alisema.
“Sasa tunatakiwa kupata pointi nyingi iwezekanavyo ili tupate nafasi ya nne, kisha tujiandae kuanza vema msimu ujao kutwaa ubingwa.

“Tulianza vibaya, na tumepata pointi nyingi, lakini katika mechi za maamuzi (matokeo) yametuhukumu.”
Licha ya mtazamo mbaya, Allegri amewatetea wachezaji wake kwa kusema walicheza vizuri wakati wote wa mchezo dhidi ya Inter Milan.

“(Ilikuwa) mechi nzuri – walicheza vizuri – tulitengeneza nafasi nyingi na tulipiga mashuti mengi langoni,” alisema.
“Ni mbaya sana kushindwa, (lakini) kuna nafasi ya kujiboresha.”

Kwa sasa Juventus inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi ya Italia ikiwa na alama 59, ikiachwa kwa tofauti ya alama 08 dhidi ya vinara AC Milan.

Nafasi ya pili inashikwa na SSC Napoli yenye alama 66 na Inter MIlan ipo nafasi ya tatu ikiwa na alama 63.

Usajili wa Adebayor Simba SC, Mashabiki wapewa ujumbe
Van Gaal aweka wazi ugonjwa unaomsumbua