Aliyewaji kuwa Meneja wa Manchester United, Louis van Gaal amesema kwa sasa anafanyiwa matibabu ya matibabu ya saratani ya tezi dume.

Van Gaal mwenye umri wa miaka 70, amesema ameficha habari hizo kutoka kwa wachezaji wake wakati wa mapumziko ya Michezo ya Kalenda ya FIFA.

“Sikutaka kuwaambia wachezaji wangu kwa sababu ingeweza kuathiri uchezaji wao,” amesema.

Van Gaal yuko katika kipindi chake cha tatu kama kocha mkuu wa Uholanzi, akiwa ameiongoza hadi nafasi ya tatu kwenye Kombe la Dunia la mwaka 2014 na sasa kwenye fainali za Kombe La Dunia 2022 huko Qatar.

Ameongeza: “Katika kila kipindi nikiwa kocha wa timu ya taifa nililazimika kuondoka usiku kwenda hospitali bila wachezaji kujua hadi sasa, huku wakidhani ni mzima wa afya, lakini…sipo.”

Katika kipindi cha miaka miwili akiwa Man United, Van Gaal aliiongoza klabu hiyo kufanikiwa kubeba Kombe la FA mwaka 2016 kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Jose Mourinho.

Pia, amewahi kutwaa mataji ya ligi akiwa na Barcelona, ​​Bayern Munich, AZ Alkmaar na Ajax, ambapo aliiongoza timu hiyo ya Uholanzi kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 1995.

Juventus yajiondoa mbio za ubingwa Italia
Utafiti wa Gesi ya Heliam kuanza Tanzania