Johansen Buberwa, Bukoba – Kagera.

Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA Mkoani Kagera, umeiomba Serikali kuupatia Mkoa wa Kagera Meli kubwa ya mizigo, ili kusaidia uondokanaji wa changamoto kubwa kwa baadhi ya Wafanyabiashara wanaotumia njia za panya kupititisha bidhaa zao mipakani, na kukosesha mapato ya Nchi.

Akizungumza kwa niaba ya Kamishina M kuu wa Mamlaka hiyo wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya mtoa shukrani kwa wateja Mkoani humo, Naibu Mkurugenzi wa Fedha na Makusanyo ya kodi na yasiyo ya kodi, Ramadhani Sengati amesema kwa sasa wamechukua jukumu kubwa la pambana na changamoto hizo kwa kuanza kutoa elimu kwa mlipa kodi.

Akijibu hoja hiyo, Mkuu wa Mkoa Kagera, Hajath Fatma Mwasa amesema Serikali imeshatenga kiasi cha fedha kwa ajiri ya kuboresha Bandari ya Bukoba zaidi ya Bilioni 39 na Meli ya mizigo inaendelea kujengwa katika jiji la mwanza na itafanya kazi zake na Mkoani Kagera mara baada ya kukamilika kwa ujenzi huo na uongozi wa Mkoa unaendelaa na mikakati inayolenga kuinua uchumi.

Awali, Meneja wa TRA Mkoa wa Kagera, Mwita Ayubu amesema kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/2024, mamlaka hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Julai, Agosti na Septemba wamefanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi 28.37 Bilioni ambazo ni sawa na asilimia 99.1.

Maadhimisho ya Uhuru: Katavi waanza kwa kupanda Miti
Mikakati miwili kuibeba Mtibwa Sugar Ligi Kuu