Waziri wa nishati, Medard Kalemani amewataka Tanesco kutoa taarifa kwa wananchi pindi wanapokuwa wanafanya marekebisho ya mitambo yao ili kuzuia usumbufu kwa wananchi pindi umeme unapokatika.
Ameongezea kuwa wanapofanya marekebisho yao kwenye mtambo mmoja wahahakishe hawazimi gridi nzima ya taifa kuepusha eneo kubwa la taifa kukosa umeme kwa kipindi cha marekebisho.
-
Kitabu chenye utata kuhusu Rais Trump kuingia sokoni
-
Ndalichako amsweka ndani Meneja TBA Kigoma
-
Magazeti ya Tanzania leo Januari 5, 2018
Kalemani amekemea tabia ya Tanesco kuchukua muda mrefu kufanya marekibisho pindi hitilafu zinapotokea kwenye mitambo, na ameshauri kuhakikisha kuna vifaa vya ziada ndani ya nchi kuepuka usumbufu wa kukaa muda mrefu kusubiria kuagiza vifaa hivyo nje ya nchi.
Aidha ameitaka Tanesco na Songas kuanza kugawana mapato kwa usawa kulingana na mkataba uliopo baina yao, na amekiri kuwa hakuna usawa kwenye mgawanyo wa mapato.
Ameeleza serikali na TFDL kwa ujumla wana hisa asilimia 36, lazima kuwe na usawa katika ugawaji wa mapato, TANESCO na Songas wanatakiwa wakae kwa pamoja waliangalie kimkataba