Mwandishi wa kitabu chenye utata kuhusiana na rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa amekabiliana na vikwazo kutoka kwa wanasheria wa rais huyo wanaojaribu kuzuia kisichapishwe.

Kitabu hicho kijulikanacho kwa jina la Fire and Fury kilichoandikwa na Michael Wolff kutokana na upinzani mkali wa uchapishwaji wake kwa sasa kinatolewa siku nne kabla ya muda uliotarajiwa.

Aidha, Mwandishi wa kitabu hicho amethibitisha kupitia ukurasa wake wa Twitter kwamba kitabu hicho kitakuwa sokoni mapema hii leo.

“Kwa sasa mambo tayari, mtakisoma kesho, asante sana Trump,” amesema mwandishi huyo wa kitabu kinachokwenda kwa jina fire and furry.

Hata hivyo, mambo yanayomhusu rais Trump na familia yake yaliyozungumzwa ndani ya kitabu hicho, yametolewa na aliyekuwa msaidizi wake, Steve Bannon zikiwemo tuhuma za familia ya Trump kukutana na watu kutoka Urusi ili kuingilia masuala ya uchaguzi wa mwaka jana.

 

Video: Vilio vyatawala, Meya Ukawa afichua siri kura aliyovuna CCM
Ndalichako amsweka ndani Meneja TBA Kigoma