Kamati ya kuhamasisha timu ya Taifa ya vijana ‘Serengeti Boys’ imeweka wazi mpiango yake itakayotumika kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri kwenye fainali za Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 zitakazofanyika nchini Gabon mwezi Mei mwaka huu.

Serengeti Boys kwa sasa ipo kambini ikiendelea na maandalizi ya michuano hiyo ambayo huenda ikawavusha hadi kwenye fainali za kombe la dunia, ambazo zitafanyika baadae mwaka huu nchini india.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Charles Hilary amesema mchakato wa kuichangia Serengeti boys upo wazi, na si fedha tu zinazohitajika bali hata huduma mbalimbali za kijamii.

“Tayarui tumeyafikia baadhi ya makampuni na yameonyesha nia ya kutusaidia, tunaendelea kufanya mawasilino na makampuni mengine” Amesema Hilary

Amesema hawatarajii fedha pekee, bali vitu vingine mbalimbali kama chakula na tiketi za ndege zitakazokua na msaada kwa timu hiyo.

Zanzibar Yapeta Mkutano Mkuu CAF
Roy Keane Awashushia Zigo la Lawama Wachezaji wa Man City