KAMISHENI ya mchezo wa ngumi za kulipwa Tanzania (TPBC) imevitaka vikundi na asasi zinazojishughulisha na usimamizi na utaratibu wa mchezo wa ngumi za kulipwa nchini kuacha mara moja kwani ni kinyume na sheria,kanuni na taratibu za mchezo huo.

Hayo yamesemwa leo na Rais wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBC) Bw.Chaurembo Palasa wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.

“Kumekuwa na vyama, asasi na vikundi ambavyo vimesajiliwa Brela lakini havikufata taratibu za sheria wala hawana vibali vya kuendesha mchezo wa ngumi nchini kutoka kwetu, tunawataka kuacha mara moja kwani ni kuvunja sheria”.

Aidha Chaulembo alisema vyama hivyo kuwa ni hewa kwani hakuna sheria, kanuni za mchezo huo za mwaka 1967, 1971 na 1999 zinazowatambua kuwa ni wasimamizi na waratibu mchezo wa ngumi za kulipwa nchini.

Kwa upande wake Katibu msaidizi wa kamisheni hiyo Bw.Chatta Michael amewataka wadau wa mchezo wa ngumi za kulipwa nchini kuwa na leseni na vibali toka katika kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini ambapo alitaja tarehe ya mwisho kutoa vibali hivyo ni Octoba 19 mwaka huu.

Aidha Chatta aliwataka waandaaji wa mapambano ya ngumi za kulipwa kuomba vibali vya uandaaji wa mapambano hayo angalau siku kumi na nne(14) kabla ya pambano.

Akifafanua zaidi alisema waandaaji hao pia wanatakiwa kubainisha maeneo watakayotumia,uzito wa bondia, mkanda unaoshindaniwa,utaifa wa bondia,wasimamizi wa mchezo na malipo kwa mabondia husika.

Aliongeza kuwa kamisheni inatoa pongezi kwa wadau wote wa mchezo wa ngumi za kulipwa nchini wakiwemo mabondia, waamuzi, makocha, wakufunzi, viongozi wa makampuni na taasisi zinazojiusisha na mchezo wa ngumi za kulipwa nchini kwa kuendeleza mchezo huu.

Waziri Nape Akutana Na Naibu Waziri Wa Utamaduni Kutoka Iran
Stand United FC Yang'ang'ana Na Ndoa Iliyovunjika