Mshambuliaji Harry Kane jana usiku aliibuka shujaa katika uwanja wa Wembley baada ya kufunga bao pekee lililoifanya timu ya Uingereza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Slovenia .
Kane ambaye ni nahodha wa Uingereza aliisaidia timu yake kupata goli hilo baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Kyle Walker dakika ya 90 na kupachika mpira kimiani. Goli hilo linakua la 11 katika michezo 22 aliyocheza Kane katika timu yake ya taifa.
Uingereza ilihitaji pointi mbili tu katika michezo yake miwili ya mwisho ili kufuzu lakini sasa imejihakikishia kucheza kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi baada ya kukusanya pointi zote tatu katika mchezo wa jana.
-
Facebook kuonyesha ligi ya Uingereza?
-
Argentina, Uruguay kuandaa kombe la dunia 2030
-
Daktari wa Argentina aweka wazi hali ya Aguero
Katika mchezo wa mwisho utakaopigwa Jumapili Uingereza ambayo inaongoza kudi ‘F’ ikiwa na pointi 23 itakabiliana na Lithuania.
Kocha wa Uingereza Gareth Southgate amesema kufuzu mapema kwa timu yake ni faida kwani wanaweza kupanga vizuri ni namna gani wataingia katika michuano hiyo mikubwa kwa upande wa soka duniani.