Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemtaka Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe kujisalimisha kwa Mkuu wa Polisi Mkoa wa Lindi kutoa maelezo kuhusu kauli alizozitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika viwanja vya mkapa Garden, Kilwa Masoko.
Aidha, Lugola ametoa agizo hilo leo tarehe 31 Julai, 2018 jijini Dar es Salaam, ambapo amesema makosa ya Zitto ni pamoja na kufanya mkutano kwenye jimbo lilisilo la kwake na kutoa maneno ya uchochezi.
“Juzi katika Jimbo la Saidi Bungara, Zitto alikaidi agizo la kutokufanya mkutano wa hadhara na kwenda kufanya mikutano katika jimbo lisilo la kwake, Zitto mahali popote alipo ajisalimishe kwa mkuu wa polisi mkoa wa Lindi na endapo asipojisalimisha ndani ya siku mbili nitamulekeza IGP ili popote alipo akamatwe,” amesema Waziri Lugola.
Hata hivyo, katika hatua nyingine, Lugola amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kumchukulia hatua Mkuu wa Polisi Wilayani Kilwa (OCD) kutokana na kumruhusu Zitto kuendelea kufanya mkutano katika jimbo lisilo la kwake.
-
Mahakama yalitoa MwanaHalisi kifungoni, lakutana na kiunzi kingine
-
Mahakama yamnyooshea kidole Mbowe
-
Mkuu wa Wilaya ya Hai aapishwa