Chelsea inawakaribisha Man Utd leo katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza EPL utakaopigwa kwenye dimba la Stamford Bridge huku kukiwa na taarifa za kurejea kwa kiungo wa kati N’Golo Kante ambaye amekuwa nje kwa mechi sita akisumbuliwa na jeraha la nyonga.

Kikosi cha Antonio Conte kimeruhusu kufungwa jumla ya mabao 11 katika michezo 6 ambayo kimecheza bila kuwa na N’Golo Kante lakini kurejea kwa kiungo huyo kutaisadia Chelsea kwenye mchezo wa leo hasa sehemu ya ulinzi.

Kocha Jose Mourinho anarejea katika dimba la Stamford Bridge huku akiwa na kumbukumbu ya kupokea  kipigo cha mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu uliozikutanisha Chelsea na Man Utd msimu uliopita huku Kante  akifunga moja ya mabao hayo.

United waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa marejeano wa ligi kuu wakicheza katika uwanja wa Old trafford na leo ni mchezo wa tatu unawakutanisha Antonio Conte na Jose Mourinho.

Chelsea wako katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa EPL wakiwa na pointi 19 baada ya kucheza michezo 10 huku Man Utd wakiwa nafasi ya 2 kwa pointi 23 baadaya kucheza michezo 10.

 

 

 

Wafuasi 12 wa Chadema watiwa mbaroni
Marekani yaishambulia ISIS Somalia