Operesheni maalumu ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini, iliyofanyika Wilayani Arumeru Mkoani Arusha imefanikisha ukamataji na uteketezaji wa Magunia 237 ya Bangi na Mbegu zake kilogram 310, ambazo zilikuwa zimesafishwa tayari kwa kupandwa.

Akizungumza wakati wa uchomaji wa Bangi hizo Mkuu wa Oparesheni wa Mamlaka hiyo Kanda ya Kaskazini, Innocent Masangura kwa niaba ya Kamishina wa Mamlaka ya Kupambana na kudhibiti Madawa ya ya Kulevya, Aretas Lyimo ametoa wito kwa Wakazi wa Wilaya hiyo kuachana na Kilimo hicho kwa kuwa msako bado unaendelea.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Emmanuela Kaganda amesema kutokana na oparesheni walizozifanya wahusika wamebadili mbinu hivi sawa wanazificha nyumbani na kwenye makorongo na si mashambani kama ilivyokuwa hapo awali.

Amesema, kwa sasa wanaendelea na utafiti wa kupata zao mbadala yatakayo stawi eneo hilo, ikiwa ni jitihada za kufanya wananchi hao waache na Kilimo hicho, huku uongozi wa eneo hilo pamoja na Wananchi wakipongeza zoezi hilo kwa kueleza jinsi Vijana walivyoathirika na matumizi ya Bangi yenye uhusiano na suala la momonyoko wa maadili.

Jude Bellingham anogewa Real Madrid
Robertinho apewa mbinu za kuibwaga Al Ahly