Kemikali yenye sumu ya methanol imetambuliwa kuwa chanzo cha vifo vya vijana 21 waliofariki katika baa ya Enyobenio iliyopo mjini London Mashariki mwa nchi ya Afrika Kusini Juni 26, 2022.

Naibu Mkurugenzi wa Mkoa wa Eastern Cape Huduma ya kliniki, Dkt. Litha Matiwane amesema kemikali hiyo ya Methanol imegunduliwa kwa miili yote 21 iliyokutwa eneo la tukio na kudai kuwa bado kuna uchanganuzi wa kimaendeleo wa viwango vya kiasi vya methanol na kama inaweza kuwa chanzo cha mwisho cha vifo.

“Bado matokeo haya yanasubiri matokeo ya mwisho ambayo yanafanywa katika maabara katika jiji la Cape Town, lakini uchunguzi umeonesha ipo kemikali hii katika miili yote 21 iliyofanyiwa vipimo,” alisema Dkt. Matiwane.

Rais wa Afrika ya Kusini, Cyril Ramaphosa, Waziri Mkuu wa Eastern Cape Oscar Mabuyane, Meya wa BCM Xola Pakati na Waziri wa Polisi Bheki Cele walikuwa baadhi ya watu mashuhuri katika mazishi ya vijana 21 waliofariki nchini humo.

Methanol, ni aina ya pombe yenye sumu ambayo hutumiwa viwandani kutengenezea, dawa ya kuua wadudu au chanzo mbadala cha mafuta na haitumiwi katika uzalishaji wa pombe inayouzwa kwa matumizi ya binadamu na bado haijajulikana ni jinsi vijana hao walivyomeza dawa hiyo ya methanoli.

Mathinawe amesema, sumu ya pombe na kuvuta hewa ya kaboni monoksidi vyote vimeondolewa kama sababu zinazoweza kusababisha vifo ingawa athari za wote ziligunduliwa katika miili ya waathiriwa wote 21.

Vijana hao, walifariki katika mkahawa wa Enyobeni katika kitongoji cha Scenery Park Mashariki mwa London asubuhi ya Juni 26, hali iliyoshtua nchi na kusababisha uchunguzi wa polisi na mamlaka ya leseni za vileo.

Waombolezaji wakiwa wameshikilia picha za wapendwa wao waliopoteza maisha.

Wengi wa vijana hao, wenye umri wa kati ya miaka 13 na 17, walipatikana wakiwa wamekufa katika tavern hiyo, huku miili yao ikiwa imetapakaa kwenye meza na makochi na wengine walifariki baada ya kufikishwa katika vituo vya afya vilivyo karibu.

Polisi wa Afrika Kusini, wataongozwa na matokeo ya mwisho ya uchambuzi wa sumu ili kubaini iwapo mtu yeyote atakabiliwa na mashtaka ya uhalifu kwa vifo hivyo 21, waziri wa Polisi wa kitaifa Bheki Cele amesema.

Mmiliki wa tavern ya Enyobeni, na baadhi ya wafanyakazi walikamatwa na kwa sasa wako nje kwa dhamana huku wakikabiliwa na mashtaka yanayohusiana na ukiukwaji wa sheria za biashara ya vileo ikiwemo uuzaji wa vileo kwa watoto.

Hali ilivyokuwa nje ya baa ya Enyobeni siku ya tukio.

Nina uhakika wa ushindi: Naibu Rais

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa alizungumza katika mazishi ya misa ya vijana na kuapa serikali yake itachukua hatua kuzuia pombe kutolewa kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 18.

Wagombea wenza 'watifuana' katika mdahalo
Mahakamani kwa kuwaimbisha watoto ubaguzi