Raia wa Uchina, Lu Ke anayeshutumiwa kwa ubaguzi wa rangi na kuwanyanyasa watoto nchini Malawi ameshtakiwa kwa ulanguzi wa binadamu katika mji Mkuu nchi hiyo Lilongwe, Julai 18, 2022..

Raia huyo, Lu Ke (26), alikamatwa mwezi uliopita katika nchi jirani ya Zambia kwa kuingia kinyume cha sheria baada ya kutoroka Malawi wakati madai ya unyanyasaji dhidi yake yalipoibuka.

Ke, anadaiwa kuwarekodi watoto wakiimba nyimbo za ubaguzi wa rangi kwa lugha ya Kichina ambayo hawakuielewa, na kisha kuuza video hizo kwenye mitandao ya kijamii ya Jamhuri ya Uchina.

Sehemu ya kipande cha Video kilichosambaa katika mitandao ya kijamii, kikionesha maneno ya kibaguzi kwa lugha ya kichina yaliyowekewa tafsiri ya Kiingereza waliyoimbishwa Watoto nchini Malawi, bila kufahamuu maana yake.

Mara baada ya kukamatwa, Ke alirejeshwa nchini Malawi na alifikishwa Mahakamani Julai 18, 2022 ambapo alishtakiwa kwa makosa matano ya kusafirisha watu ambapo Waendesha mashtaka wa Serikali wanasema mashtaka zaidi yanatarajiwa kufunguliwa uchunguzi utakapokamilika baada ya wiki mbili.

Hata hivyo, Hakimu Mwandamizi wa Mahakama ya Lilongwe, James Mankhwazi alimnyima dhamana Ke akiteta hoja ya waendesha mashitaka walio onesha kuwa mshtakiwa anaweza kukimbia, kutokana na kutokuwa na mahali maalum pa kukaa na anaweza kuharibu uihahidi kwa kuwahadaa watoto hao.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali wa Malawi, Prescott Mwayiulipo naye alipinga Kortini suala la kumwachilia Ke kwa dhamana, akidai hatua hiyo itasaidia kumlinda dhidi ya watu waliokasirishwa na video hizo.

Wazazi waliojitokeza nje ya Mahakama Kuu jijini Lilongwe nchini Malawi wakati mshtakiwa Ke akisomewa mashitaka.

Katika taarifa yake ya mwezi jana, Ubalozi wa China nchini Malawi, ulilaani kitendo cha mshtakiwa na kusema Serikali ya China haiwezi kuvumilia vitendo vya ubaguzi wa rangi.

Mtuhumiwa Lu Ke, raia wa Uchina anayeshikiliwa nchini Malawi mara baada ya kutorokea nchini Zambia.

Kemikali yenye sumu yatambuliwa katika miili ya Vijana 21
Sirro aondolewa Jeshi la Polisi, mrithi wake atangazwa