Zikiwa zimesalia takriban siku 20 kabla ya uchaguzi mkuu nchini Kenya, mgombea Urais Raila Odinga na mgombea mwenza wake Martha Karua wamesema wana uhakika wa ushindi.

Odinga na Karua walikuwa wakizungumza mbele ya vyombo vya habari vya kigeni kuhusu kampeni yao ya pamoja ambapo aawili hao pia walijibu maswali kuhusu mipango yao ya kukabiliana na ufisadi.

“Nadhani hatua ya kwanza katika kukabiliana na ufisadi ni kueleza nia yetu wazi, ambayo tumefanya, kulingana na maneno yetu na matendo yetu, ambayo yatawaaminisha wananchi kwamba tunazingatia na itawatia moyo wananchi kujiunga na vita dhidi ya ufisadi,” alisema Karua, mgombea mwenza wa Odinga na mwanasiasa mkongwe wa Kenya.

Raila Odinga

Baada ya majaribio mengi bila mafanikio, kiongozi mkongwe wa upinzani Odinga anawania tena urais wa Kenya ambapo safari hii anaungwa mkono na rais anayemaliza muda wake.

“Katika mchakato huo tulikutana, tukajadiliana, tukakubaliana kuwa nchi ni kubwa kuliko sisi sote na tutembee pamoja ili kuleta nchi pamoja na kuleta amani ili nchi ipate maendeleo zaidi,” alisema Odinga wakati akijibu swali kuhusu uhusiano wake na Rais Uhuru Kenyatta.

Ili kushinda uchaguzi huo, muungano wa Azimio La Umoja wa Odinga lazima uzuie ushindani mkali kutoka kwa mpinzani Naibu Rais William Ruto.

William Ruto

Chaguzi za urais, wabunge na serikali za mitaa zinafanyika wakati ambapo nchi hiyo yenye uchumi mkubwa zaidi Afrika ya Mashariki ikikabiliwa na athari zinazosababishwa na janga la Uviko-19 na vita vya Urusi na Ukraine.

Nina uhakika wa ushindi: Naibu Rais
Umeme Kagongwa ni wiki mbili