Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi, Mhandisi Ezra Chiwelesa ameitaka jamii kwa kushirikiana na wadau pamoja na Serikali kulichukulia suala hilo kama dharula na kutoa msaada wa haraka.

Akiongea katika Bweni la Wasichana lililoteketea kwa moto katika Shule ya Sekondari Mubaba iliyopo kata ya Kaniha Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera, Mbunge Ezra amesema wadau wanatakiwa kuendelea kutoa msaada ili kuweza kuwasaidia wanafunzi hao kuendelea na masomo.

“Kamati ya ulinzi na usalama imemteua katibu tawala wa Wilaya hiyo kuwa Mratibu na mpokeaji wa misaada hiyo na hapa natoa magodoro 50 na pia mgodi wa Stamico wameotoa magodoro 50 pamoja na kampeini ya Alsamood ya wilayani Biharamulo waliotoa mashuka Zaidi ya 280 kwa wanafunzi hawa,” amesema.

Bweni la Wasichana lililoteketea kwa moto katika shule ya Sekondari Mubaba iliyopo kata ya Kaniha Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera.

Mkuu wa wilaya Biharamulo, Kemilembe Lwota amesema kutokana na dharula iliyopo tayari ameshatoa maagizo ya kuanza kwa ujenzi wa bweni hilo haraka na kusisitiza kuwa kufikia jumamosi ya Julai 23 Mwaka huu wanafunzi wawe wameingia katika bweni hilo.

Kemilembe amewataka Wanafunzi kuendelea kuwa wavumilivu katika kipindi hiki wakati Serikali ikishughulikia tatizo linalowakabili na kuwataka Wazazi kuwa na amani kwani watoto wao wapo salama na kwamba vyombo vya ulinzi na usalama bado vinafanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huo.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Mkuu wa shule hiyo Mwalimu, Alfred Katobesi amesema Julai 17, 2022, moto ulioteketeza Bweni la Wasichana hao, ulianza majira ya saa 12 jioni wakati wanafunzi wote wakiwa wameenda kupata chakula Cha usiku.

Amesema, moto huo umeteketeza mali zote za wanafunzi yakiwemo magodoro, vitanda, nguo, Madaftari na kuwaacha wakiwa hawana la kufanya waka kuwa na msaada wowote hali iliyowapelekea wengi wao kulala madarasani.

Kwa upande wao, wanafunzi hao wameiomba Serikali kuwapa msaada kutokana na ajali hiyo kuwathiri kwa kiasi kikubwa huku wakitoa shukurani zao kwa hatua za awali ambazo zimeshaanza kuchukuliwa ikiwemo kupatiwa msaada huo.

Aidha katika hatua nyingine wamesema Serikali iwasaidie kuwajengea Mabweni mengine ili kupunguza msomgamano katika bweni lililouungua ambalo lilikuwa likibeba wanafunzi 135 huku uwezo wake ukiwa ni kubeba wanafunzi 108.

Sehemu ya uharibufu katika Bweni lililoteketea kwa moto Shule ya Sekondari Mubaba iliyopo kata ya Kaniha Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera.

Serikali matatani kwa kuwabagua Ogiek
UN yataka uchunguzi vifo 23 vya Waafrika