Serikali imewataka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), kukusanya maoni kwa wananchi ili kubaini sababu zinawafanya wengi wao kutoandika wosia.

Wito huo, umetolewa na Serikali hii leo Julai 18, 2022 jijini Arusha, kupitia kwa Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Mary Makondo ambaye amebainisha kuwa ipo haja ya kutambua chanzo cha mwamko huo mdogo ili kuweza kutatua tatizo hilo.

Mary, ambaye alikuwa akizungumza wakati wa mkutano wa mamlaka hiyo na wadau amesema, licha ya hamasa ambayo imekuwa ikitolewa juu ya umuhimu wa wosia ambapo ni idadi ndogo ya watu ambao huandika wosia.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mary Makondo.

“Tunawaelekeza Rita kuandaa dodoso ili ipelekwe kwa wananchi waeleze sababu zinazofanywa washindwe kuandika wosia, tumefika huku maana migogoro imekuwa mingi ambayo ingeweza kuzuilika iwapo wosia ungeandikwa,” amesema Katibu Mkuu.

Amesema, suala la kuandika wosia halina uhusiano na mambo ya imani potofu bali huweka mazingira mazuri ya wale unaowaacha pindi mtu anapoaga Dunia.

Awali, Mtendaji Mkuu wa RITA, Angella Anatory aLIsema mamlaka hiuo imepokea wosia 700 pekee idadi ambayo ni ndogo ikilinganishwa na takwimu za namba ya watanzania.

Wakili Mkuu wa serikali, Gabriel Malata akizungumza katika ufunguzi  wa mafunzo hayo jijini Arusha.

“Zipo taasisi nyingine zinazohusika katika uandaaji na utunzaji wa wosia kama Wanasheria binafsi, lakini upande wa Serikali, RITA ndio hufanya kazi hiyo hivyo niwasisitieze Watanzania kujenga mazoea ya kandika wosia,” amebainisha Mary.

Hata hivyo, ametoa maelekezo kuwa Wizara inayafanyia kazi suala hilo kwa kuandaa dodoso ya ndani ili ipitiwe na Utawala kabla ya kuipeleka kwa wananchi na kupata maoni juu ya uzito wa kuandika wosia ambao ni muhimu kwa familia.

Naye, Wakili Mkuu wa Serikali Gabriel Malata amesema ofisi yake imeshiriki kikamilifu katika kukuza uchumi ikiwemo kushiriki kwenye utatuzi wa migogoro na mashauri kwa wakati na kwa kushirikiana na vyombo vya utoaji haki.

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro.

“Tumeendesha mashauri ya madai na usuluhishi kwa weledi kwa niaba ya serikali na Taasisi zake na kuokoa fedha na mali nyingine za serikali, ambazo watu wasiostahili wangeweza kulipwa na zaidi tumeokoa zaidi ya Sh.Trilioni 10,”amesema.

Malata ameongeza kuwa, endapo Serikali ingeshindwa katika mashauri hayo ingewajibika kuwalipa wadai fedha hizo na kushindwa kutoa huduma na kukuza uchumi kwa kutumia fedha hizo.

Licha ya mafanikio hayo bado zipo changamoto ya upungufu wa watumishi wenye stadi maalumu katika maeneo mtambuka kama mafuta na gesi, usuluhishi wa kimataifa na majadiliano

Ajali ya ndege Somalia, 30 wanusurika kifo
Ni Homa ya Mgunda mlipuko wa ugonjwa Lindi