Watu 30 wamenusurika kifo, baada ya ndege ya shirika la ndege la Jubba kuanguka wakati ikitua katika uwanja wa ndege wa Aden Adde katika mji mkuu wa Somalia.

Mamlaka zinasema, watu hao wakiwemo abiria wote na wafanyakazi waliokuwa ndani ya ndege hiyo wameokolewa.

Ndege iliyopata ajali Somalia.

Baada ya ajali hiyo, wafanyakazi wa uwanja huo wa ndege walikusanyika kufanya kazi ya kusafisha njia ya ndege ili ndege nyingine zipite kwa usalama.

Televisheni ya taifa la Somalia, limefanikiwa kusambaza picha za moshi mkubwa na moto kutokana na ajali hiyo.

UNFPA yawaonesha MSD umuhimu wa 'kila ujauzito'
Serikali yataka maoni watu kutoandika wosia