Serikali nchini Kenya imepitisha muswaada wa sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi ambayo itawabana watumishi wa umma wanaotoa taarifa binafsi za wateja wao.
Sheria hiyo inasema Mtumishi wa umma ambaye atashiriki katika kutoa taarifa binafsi za mteja kwa mtu mwingine, atatozwa faini ya zaidi ya Tsh. Milioni 11 au kifungo cha miaka miwili jela au vyote kwa pamoja.
Mswaada huo wa sheria ya ulinzi wa Taarifa ya mwaka 2019 uliwasilishwa jana na kutiliwa saini na Rais uhuru Kenyatta.
Inatoa msingi wa kisheria wa ulinzi wa faragha ya mtu katika hali zote ikiwemo habari binafsi zinazokusanywa na kuhifadhiwa kutumiwa na mtu mwingine.
Sheria hiyo inayataka Makampuni na mashirika kabla ya kutoa taarifa za wateja wao kwa wtu wengine ni lazima wapate kibali au ruhusa ya mteja husika.