Mwanamuziki wa bongo fleva Alikiba amemjibu shabiki wa Diamond Platnumz aliyejitokeza wakati akizungumza na waandishi wa habari jana usiku na kumkabidhi penseli.

Shabiki huyo alimuomba Alikiba kuacha ugomvi na mwanamuziki mwenzie huku akimkabidhi penseli ambayo ilidaiwa kuwa mfano wa chanzo cha ugomvi wao.

Katika kulijibu hilo Alikiba amesema kwa sasa hana ugomvi na Diamond lakini hawezi kushiriki kwenye matamasha ya muimbaji huyo kwa kuwa na yeye anashughuli zake nyingi za kufanya.

Pia hit maker huyo wa Aje amesema tayari alishamkatalia Diamond kushiriki kwenye matamasha yake lakini bado muimbaji huyo anaendelea kumtaja sana.

CHAUMA waunga tela kususia uchaguzi
Kenyata asaini mswaada sheria ya ulinzi wa taarifa

Comments

comments