Aliyekuwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema hatafaulu kuhudhuria mazungumzo ya amani kuhusu Ethiopia ambayo yanafanyika nchini Afrika Kusini.

Mazungumzo hayo ambayo yameratibiwa kuanza Oktoba 09, huko Afrika Kusini lakini Kenyatta anasema ana shughuli nyingi na hivyo hatafika Afrika Kusini yatakapofanyika mazungumzo hayo.

Uhuru amemwandikia mwenyekiti wa kikao hicho Musa Faki akisema kikao cha kesho kimewiana na shughuli zake, “Naomba nijulishe ofisi yako kwamba sitaweza kuhudhuria kikao cha kesho cha amani kuhusu muungano wa Afrika kilichoratibiwa kufanyika Oktoba 8 nchini Afrika Kusini kutokana na shughuli zingine,” alisema Kenyatta.

Uhuru pamoja na aliyekuwa rais wa Nigeria Oleseguun Obasanjo walikuwa wameratibiwa kuongoza mazumzo hayo ambapo suluhu la uhasama kati ya serikali ya Ethiopia na Tigray linatafutwa na Uhuru alisema ni lazima milio ya Risasi isimame.

Wakati wa utawala wake kama rais, Uhuru alichukua nafasi muhimu katika mazungumzo ya amani nchini Ethiopia, Sudan Kusini, DR Congo na Somalia.

Katika hotuba yake, Ruto aliahidi kuendelea na mipango ya amani iliyokuwa ikiendelezwa na Uhuru, “Kenya itaendelea kutekeleza jukumu lake katika diplomasia ya nchi mbili na kimataifa, ikithamini kwamba sisi ni wenyeji wa mashirika makubwa ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na UN. Ninajitolea kwa mipango ya amani katika eneo letu, ikiwa ni pamoja na Ethiopia na kanda ya ziwa kuu,”

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Kenya wamenena tofauti kutokana na suala hilo ambapo Mchanganuzi wa kisiasa Mutahi Ngunyi alisema kuna zaidi ya yale ambayo yametumwa kwa vyombo vya habari.

“Hesabu haziingiani kuhusu Rais Uhuru Kneyatta kukosa kuhudhuria mazungumzo ya maani ya Ethipia-Tigrey. Kwanza, Ruto alizuru Ethiopia wiki hii na kukutana na Waziri Mkuu. Pili, wakati alirejea akakutana na mwakilishi wa Marekani ambaye ndiye mpatanishi mpya,” alisema Ngunyi.

Huku Mutahi akinusa hatari kuhusiana na kinachoendelea, wandani wa Ruto wanasema hatua ya Uhuru ni kukataa kazi aliyopewa na Seneta wa Nandi Samson Cherargei amemtaka Rais Ruto kumpa Raila kazi hiyo ya kuwa balozi wa amani.

“HE Kenyatta amekataa kazi ya kuwa balozi wa amani katika mazungumzo kuhusu Ethiopia. Ni kama kazi ya kuwa mwenyekiti wa Azimio imekuwa nyingi sana. Ruto anafaa kumteua Raila kuwa balozi wa Amani katika mazungumzo hayo,” alisema Cherargei.

Rais William Ruto baada ya kuapishwa Septemba 15 alitangaza kuwa amemteua Kenyatta kuendelea kuongoza mazungumzo hayo ya kuleta amani nchini Ethiopia.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Octoba 09, 2022  
Ruto kuzuru Tanzania Oktoba 09