Uongozi wa klabu ya Florida State University, inayoshiriki michuano ya Amarican Football huko nchini Marekani, umefungashia virago mchezaji wake De’Andre Johnson, baada ya kuthibitika kuwa alimsukuma msichana katika sehemu za starehe (Bar).

Uongozi wa klabu hiyo umeridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani ambao unaonyesha Johnson alimsukuma msichana mwenye umri wa miaka 19 na kumdhalilisha katika sehemu hiyo ya starehe.Ushahidi huo ulionesha picha zilizochukuliwa katika mitambo ya kamera za CCTV.
De'Andre Johnson akimsukuma msichana
Kwa kipindi cha majuma kadhaa, mahakama imekuwa ikisiliza kesi ya mchezaji huyo kufuatia tukio hilo la Juni 24 mwaka huu. Jana, mahakama ilieleza kuwa imejiridhisha na ushahidi na kumtia hatiani mchezaji huyo.

Kabla ya kufanyika kwa maamuzi ya kufukuzwa klabuni hapo, Johnson alikuwa amesimamishwa kupisha kesi inayomkabili, na sasa imedhihirika hatokuwa sehemu ya wachezaji ambao wanaunda kikosi cha Florida State University.

Uongozi Wa Wembley Wakanusha Kupokea Ofa Ya Chelsea
Mayweather Avuliwa Ubingwa Wa Dunia