Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu, wameshindwa kufika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa kile kilichoelezwa ni changamoto ya usafiri wa gari la magereza.

Mbowe na wenzake wanakabiliwa na mashtaka sita yakiweno ya kufadhili vitendo vya ugaidi na kukusanya pesa kwa ajili ya kufanya vitendo vya kigaidi, katika kesi ya Uhujumu Uchumi namba 63/2020.

Mashtaka mengine ni kula njama za kutenda makosa, kukutwa na silaha aina ya bastola, risasi pamoja na sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kinyume cha sheria.

Mbali na Mbowe, ambaye ni mshtakiwa wanne katika kesi hiyo, wengine ni Halfan Hassan, Adam Kasekwa na Mohamed Lingwenya.

Kutokana na hali hiyo, kesi hiyo imeendeshwa kwa njia video huku washtakiwa watatu (Mbowe, Hassan na Lingwenya) wakiwa Gereza la Ukonga na Kasekwa akiwa Gereza la Segerea.

Kutokana na hali hiyo, mahakama imelazimika kusikiliza kesi hiyo mara mbili, kwa washtakiwa waliopo Ukonga kisha kuhamia Gereza la Ukonga aliko Kasekwa.

Awali, jopo la mawakili watatu wa upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Pius Hilla, umedai kesi hiyo iliitwa kwa ajili ya kutajwa.

Wakili Hilla baada ya kueleza hayo, kiongozi wa jopo la mawakili wa utetezi, Peter Kibatala amedai alitarajia wateja wake wapelekwe mahakamani kwa kuwa wamewasilisha taarifa ya kusudio la kuiomba mahakama hiyo kuipeleka Mahakama Kuu kama suala la kikatiba kutokana na matamshi yaliyotolewa na taasisi moja nchini.

Kibatala amesema kuwa taasisi hiyo ambayo hakutaka kuitaja kuwa imeingilia uhuru wa mahakama.

Hata hivyo, Hakimu Simba baada ya kusikiliza hoja za pande, ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 27, 2021 itakapoitwa kwa ajili usikilizwaji.

Katibu mkuu wa CCM atoa pongezi kwa wakandarasi
Kibadeni: Simba SC haina jeuri ya kukataa