Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amewapongeza wa simamizi na wakandarasi wanaoendelea na ujenzi wa daraja la Tanzanite lililokuwa likifahamika kama daraja la salender lililopo Dar es slaam.

Ameyasema hayo leo alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo katika ziara iliyojumuisha wajumbe wote wa  Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

Mwenyekiti wa kampuni za Asas afariki dunia

Aidha, ameipongeza TANROAD kwa usimamizi mzuri na  kuhusishwa kwa wananchi na wakandarasi wengi wazawa huku akitoa maelekezo kuwa ni muda mwafaka sasa kuwepo na programu maalum ya kukuza na kuwajengea uwezo wakandarasi wazawa ili fursa za kandarasi za ujenzi zinazoendelea hapa nchini baadaye ziweze kufanywa na wazawa.

Awali akiwasilisha taarifa ya mradi huo, Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Rogatus Mativila ameeleza kuwa ujenzi huo umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 243.7 na sasa umefikia asilimia 91. Ameongeza kuwa asilimia 92 ya wafanyakazi katika mradi huo unaotarajiwa kukamilika Desemba 2021 ni wazawa.

Ulega awahasa wakulima na wafugaji
Kesi ya Mbowe yaahirishwa