Beki wa kati wa klabu ya Ajax Amsterdam Kevin Veltman ameonyesha kuisubiri kwa hamu safari ya kuelekea jijini London, baada ya kuhusishwa na taarifa za kuwindwa na wagonga nyundo wa jijini London (West Ham Utd).

Juma lililopita vyombo vya habari vya nchini Uholanzi viliibuka na taarifa za beki huyo kuhitajika London Stadium, huku ikidaiwa kiasi cha Pauni milioni 10 kimetengwa kwa ajili ya kukamilisha mpango huo.

Baada ya mchezo wa ligi ya nchini Uholanzi ambapo Ajax walichomoza na ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya FC Utrecht hapo jana, Veltman alihojiwa na vyombo vya habari kuhusu tetesi zinazomuandama.

Alisema kwa upande wake taarifa hizo anaziona na kuzifuatilia katika mitandao ya kijamii na kwenye baadhi ya vyombo vya habari, hivyo aliomba kuachwa kwa muda, lakini akakiri kusubiri kwa haku kubwa kuona jambo hilo likitokea katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.

“Na mimi ninazisikia hizo taarifa katika vyombo vya habari, na wakati mwingie naziona kwenye mitandao ya kijamii, lakini ikitokea ninakwenda London, mambo yatakua safi kwa sababu ni hatua kubwa kutoka mahala fulani kwenda kwingine,” Alisema Veltman.

“Natarajia kuona mambo yakiwa kweli katika kipindi hiki cha siku nane zilizosalia, kabla ya dirisha la usajili halijafungwa.”

Guedes Kurithi Nafasi Ya Memphis Depay Old Trafford
Aristica Cioaba Kuisubiri Simba SC