Chama cha Haki Miliki Tanzania (COSOTA) kimetoa mchanganuo wa kiasi anachostahili kulipwa msanii na mtayarishaji wa muziki husika kutokana na kazi zake kuchezwa katika vituo vya runinga na redio ndani na nje ya nchi.

Afisa Mtendaji Mkuu wa COSOTA, Bi. Doreen Sinare ameeleza kuwa wasanii watapata asilimia 70 ya mirabaha inayotokana na kazi zao kuchezwa katika vituo hivyo lakini watapokea asilimia 60 huku asilimia 10 ikichukuliwa kama akiba itakayowekwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa faida yake ya baadaye.

Bi. Sinare alieleza kuwa COSOTA inashirikiana na kampuni ya Copyright Management East Africa Limited (CMEA) kwa kutumia vifaa vya kisasa vitakavyobainisha hesabu ya kila msanii kutokana na kazi zake kuchezwa ndani na nje ya nchi.

Hivi karibuni serikali ilieleza kuwa kuanzia Januari mwakani, wasanii wataanza kulipwa mirabaha kutokana na kazi zao kuchezwa na vituo vya redio na vituo vya runinga ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha wanapata haki stahiki ya kazi zao.

Mlinzi wa Mfalme wa Qatari Akamatwa na Fuvu la Twiga Kilimanjaro
Rais Magufuli, Dk. Slaa Walikubaliana Katika Hili