Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro linamshikilia moja kati ya walinzi wa Mfalme wa Qatari, Mfalme Sheikh Tamim bin Hamad At-Thani, baada ya kumkamata na fuvu la twiga akijaribu kulivusha kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kuelekea katika Falme za Kiarabu.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Fulgende Ngonyani jana alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa jeshi hilo linamshikilia mlinzi huyo wa mfalme wa Qatari aliyetajwa kwa jina la Jasim Mbarakke mwenye umri wa miaka 43.

“Ni kweli tuna mtu huyo kweye selo zetu, tulimkamata katika uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), na kumpeleka Arusha, lakini tumeshamrudisha Moshi na taratibu za kumfikisha Mahakamani zinaendelea,” alisema Kamanda Ngonyani.

Taarifa kutoka mjini Moshi zimeeleza kuwa mlinzi huyo wa Mfalme wa Qatari alikamatwa Disemba 18 mwaka huu na kikosi kazi kilichoundwa kwa lengo la kupambana na ujangili.

 

Sherehe za Kumuombea Lowassa Uvumilivu, Hekima Nusura Zivunjike
Kiasi watakacholipwa wasanii kwa kucheza nyimbo zao redioni na kwenye TV chawekwa wazi