Uongozi wa Mtibwa Sugar umewapa matumaini mashabiki wa klabu hiyo kwa kuwataka kutokua na wasiwasi na uwezo wa kikosi chao, kwa msimu huu 2020/21.
Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar Thobias Kifaru, amesema wana matumaini makubwa na kikosi chao na wanaamini msimu huu utakua watofauti sana.
Amesema usajili wa mchezaji kama Hassan Kessy alieachana na Nkana FC ya Zambia pamojana Ibrahim Hilika kutoka Zanzibar ni sehemu ya maboresho waliyoyafanya kikosini kwao msimu huu.
“Tumesajili wachezaji kutoka ligi bora na wana uwezo mkubwa hilo lipo wazi, tuna kijana wetu kutoka Nkana FC, Hassan Kesy tupo naye na kuna kijana mwingine ni Ibrahim Hilika yeye anapenda kufunga tu, mashabiki endeleeni kutupa sapoti.” Amesema Kifaru.
Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 9 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 22, baada ya kushuka dimbani mara 17.
Tayari uongozi wa klabu hiyo ya mkoani Morogoro umeshamtangaza kocha kutoka nchini Rwanda Hitimana Thiery kuwa kocha mkuu, baada ya kuondoka kwa kocha mzawa Zueir Katwila alietimkia Ihefu FC.
Hitimana anatarajiwa kuanza kazi rasmi mzunguuko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara juma hili, akichukua kijito kutoka kwa mchezaji wa zamani wa Mtibwa Sugar Vicent Barnabas aliekua anakaimu kama kocha mkuu.